Isaiah 27

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

1 aKatika siku ile, Bwana ataadhibu kwa upanga wake,
upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,
ataadhibu Lewiathani
Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.
yule nyoka apitaye kwa mwendo laini,
Lewiathani yule nyoka mwenye kujipinda;
atamuua joka huyo mkubwa sana wa baharini.

2 cKatika siku ile: “Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

3 dMimi, Bwana, ninalitunza,
nalinyweshea maji mfululizo.
Ninalichunga usiku na mchana
ili mtu yeyote asije akalidhuru.

4 eMimi sijakasirika.
Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!
Ningepambana dhidi yake katika vita,
ningeliichoma moto yote.

5 fAu niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,
wao na wafanye amani nami,
naam, wafanye amani nami.”


6 gKatika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,
Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,
naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.


7 hJe, Bwana amempiga
vile alivyowapiga wale waliompiga?
Je, yeye ameuawa
vile walivyouawa wale waliomuua yeye?

8 iKwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye:
kwa mshindo wake mkali anamfukuza,
kama siku ile uvumapo upepo wa mashariki.

9 jKwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,
nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:
Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu
kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,
hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba
zitakazobaki zimesimama.

10 kMji ulio na boma umebaki ukiwa,
makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa.
Huko ndama hulisha,
huko hujilaza,
wanakwanyua matawi yake.

11 lWakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa
nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.
Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,
kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,
Muumba wao hawaonyeshi fadhili.

12 mKatika siku ile Bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja. 13 nKatika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
Copyright information for SwhKC